Mkuu wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach ametangaza kwamba udanganyifu wa utumizi wa dawa za kulevya katika michuano ya Rio tabia hiyo itakuwa haina mahali pa kujificha.

Bw. Bach amesema kwamba wakati wa michuano hiyo maelfu ya vipimo vitafanywa na sampuli za vipimo hivyo zitahifadhiwa kwa miaka kumi ijayo na kusema kwamba atahakikisha watumizi wote wa dawa za kusisimua misuli kamwe hawatakuwa salama.

Bach Aliongeza kusema kuwa takwimu ya mwisho juu ya idadi ya wanariadha wa Urusi ambao wataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo ya michezo ya Olimpiki watatangazwa saa chache zijazo.

Wakala wa kuzuia utumizi wa dawa za kusisimua misuli imependekeza kuwa yeyote atakayekutwa ametumia dawa hizo wapigwe marufuku katika michuano hiyo chini ya mpango wa ufadhili wa serikali ingawa Kamati ya Olimpiki ya Urusi imesema kwamba wanamichezo wake wapatao mia mbili na sabini na mmoja wamesha thibitishwa kushiriki katika michuano hiyo ya Olimpiki.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *