Muigizaji wa filamu za Fast and Furious nchini Marekani, Dwayne Johnson maarufu ‘The Rock’ amesema kuwa anataka kuwania urais nchini humo.

Katika mahojiano na jarida la GQ, nyota huyo wa uigizaji anasema kuwa amelifikiria sana wazo hilo.

Anasema kwamba iwapo angekuwa rais ingekuwa muhimu na uongozi ni muhimu Kuchukua jukumu la kila mtu’.

Lakini Johnson sio nyota pekee mwenye maono ya kutaka kuhamia katika ikulu ya Whitehouse 2021.

Mark Zuckerberg , bilionea na mkurugenzi wa mtandao wa facebook pia huenda ana ndoto kama hiyo.

 

Amekuwa na mpango wa kuwatembelea raia wote wa Marekani katika majimbo 50 na amekuwa akipeperusha hewani ziara zake moja kwa moja katika mtandao wa facebook hatua ambayo inaokena kuupigia debe mtandao huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *