Kundi la The Quest Crew kutoka Magomeni Jijini Dar es Salaam limetamba kufanya maajabu yatakayofanya kuibuka na ushindi wa Dance100% mwaka 2016 kutokana na maandalizi waliyofanya.

Mwenyekiti wa kundi hilo Brown Bryton amesema wamedumu kwenye mazoezi kuanzia walipofuzu hatua ya robo fainali na katika hatua ya sasa kulingana na maelekezo ya majaji wanaamini kuibuka na ushindi bila wasiwasi wowote.

Brown amesema wana imani kwamba wenzao wamejiandaa pia ila kwa namna wao walivyojipanga kutokana na mazoezi wanayoyafanya kwasasa huku akisisitiza kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuwaondoa kwenye nafasi hiyo ya ubingwa.

Shindano hilo la Dance100% 2016 linaingia katika hatua ya nusu fainali Jumamosi hii katika viwanja vya Don Bosco Osterbay Jijini Dar es salaam.

Makundi 10 yatachuana kuweza kupatikana makundi matano ambayo yatatinga hatua ya fainali.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *