How many music icons in America and Europe have their own labels?

Je, hawana fedha za kuwekeza kwenye kumiliki lebo za muziki? Je, ni jambo rahisi sana kumiliki lebo na kuiendesha hadi kufikia mafanikio yanayotarajiwa?

Ingawa msanii mkubwa kama Usher Raymond alikuwa anamsimamia Justin Bieber na bado ameendela kuwa mshauri wake mkubwa, bado Usher hana record label yake yeye mwenyewe. Kwanini? Mbona wasanii wengine wengi sana wenye hela za kutosha kumiliki lebo zao hawafanyi hivyo?

Ni wasanii wangapi wa Kenya au Uganda ambao baada ya miaka kadhaa ya mafanikio yao wameanza kufanya biashara ya kuwasimamia wasanii wengine?

Hapa Tanzania, msanii staa na mkongwe wa bongo Fleva, Ambwene Yesaya a.k.a AY nae aliwahi kuanza shighuli hizo ili kuwasaidia wasanii wengi zaidi lakini baada ya muda mfupi akaacha kazi hiyo, kwanini?

Mkongwe Dully Sykes ana studio yake na lebo ya Dhahabu records, kwanini yuko kimya? Barnaba Classic, mbona yuko kimya?

Lakini kama vile wasanii wetu hawajifunzi, leo hii umeanza utitiri wa kila msanii kuwa na lebo yake binafsi.

Diamond Platnumz amekuja na Wasafi na ameonyesha kufanikiwa sana kwenye mradi huo mkubwa huku pia nguvu ya mafanikio hayo ikichangiwa na wasimamiaji wasanii wenye uzoefu wa muda mrefu na mafanikio ya wazi, Sallam, Babu Tale na Said Fella. Katika hali ya kuzua maswali na tafakuri ya nguvu hatimaye wasanii wengine nao wameanza kufuata nyayo za wakongwe bila ya kuuliza vizuri njia.

Huenda mafanikio ya Diamond, Platnumz yamewahamasisha sana lakini je, mastaa wetu Vanessa Mdee, Shilole, Nuhu Mziwanda na wengine wanaoanzisha lebo zao, wamejipanga?

Je, huu utitiri wa lebo za muziki zinazomilikiwa na wasanii kwenye Bongo Fleva ni ishara ya mafanikio ya Bongo Fleva au ni dalili ya mwanzo wa mwisho wa baadhi ya wasanii?

Ni kweli wasanii wengi wana uwezo wa kuwamiliki wasanii wenzao au wanatafuta watumishi wa kuwasaidia kuongeza vipato vyao?

Kumiliki lebo sio jambo dogo hivyo wasanii wasome ramani kabla ya kuanza safari, wawaulize wakongwe.

Uwekezaji wenye mafanikio kwenye uanzishaji wa lebo ya muziki unahitaji nini na nini?

Je, ni uwezo wa kifedha pekee? Je, watu gani wanahitajika kuunda timu ya mafanikio?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *