Mwanamuziki nyota wa Marekani The Game ameamuriwa na mahakama nchini humo kumlipa msichana dola milioni 7 baada ya kukutwa na hatia ya kumnyanyasa kijinsia.

Mwanamuziki huyo anadaiwa kumnyanyasa msichana huyo ambaye ni mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Priscilla Rainey kupitia kipindi chake cha runinga mwaka jana.

The Game ameamuriwa kulipa kiasi cha dola 7.13 milioni kama fidia kwa mwanamke huyo ambaye alimnyanyasa kijinsia mwaka jana.

kwa kipindi cha nyuma The Game aliandika ujumbe kupitia mtandao wa Instagram unaopinga kumlipa mwanamitindo huyo lakini kwa wakati huu aijulikani kama atamlpa mwanamke huyo au utakazia uzi wake wa kutomlipa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *