Mwanamuziki wa hip hop nchiniMarekani, The Game amepinga hukumu iliyotolewa na jaji dhidi yake kwenye kesi ya udhalilishaji na kuomba kesi hiyo isikilizwe tena.
Rapa huyo Game amesema kuwa anaimani kuwa mahakama imeonyeshwa video isiyo sahihi ya yeye na mwanamke huyo ndio maana wakatoa uamuzi kwenye kesi hiyo.
The Game hakuwepo wakati kesi hiyo inaendelea ya udhalilishaji inayomkabili mkali huyo wa hipi hop nchini Marekani.
Ikumbukwe kuwa kesi hiyo imekamilika mwezi mmoja uliopita huku jaji akiamuru The Game kulipa dola milioni $7 za Marekani.
Mlalamikaji Priscilla Rainey, alifungua kesi dhidi ya The Game mwaka 2015 akidai alidhalilishwa na mwanamuziki huyo.