Mashabiki wa hip hop nchini Marekani wamemwita The Game mbaguzi na baadhi ya baada ya kitendo cha kuwatimua wanawake weusi kutoka kwenye sherehe yake fupi baada fainali za Super Bowl.

Taarifa hiyo imeibuka baada ya dada mmoja aliyefukuzwa kwenye party hio kuweka video mtandaoni na kusema kafukuzwa sababu yeye ni mwanamke mweusi.

Baada ya tuhuma hizo The Game akajibu kwa kusema niligundua kuwa watu wengi kwenye party hio hawakualikwa na hakuna aliyekuwa anawajua kwenye kundi langu, niliwapa chakula na vinywaji na sasa wananichafulia jina.

 Kutokana na habari hizo mashabiki wamechukizwa na tabia iliyoneshwa na mwana hip hop huyo.

 Hali hiyo imesababisha mashabiki hao kumshambulia The Game kwenye mitandao ya kijamii licha ya yeye mwenyewe kukanusha taarifa hizo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *