Hekima na uungwana kamwe havina utwana,
Faraja ya Maulana daima huviandama,
Sifa hizi ziwe zetu wenye kupendana sana,
Tunaotaka umoja tuje kuzikana bwana……..
Hongera Nahreel, mwerevu na muungwana…..

Hakuna mfuatiliaji wa muziki wa bongo Fleva ambaye katika kipindi hiki hafahamu mafanikio makubwa aliyonayo nyota wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel. Mafanikio ya Nahreel yamegawanyika katika sehemu nyingi ingawa yanaweza kugawanywa katika vyanzo vyake vinavyotokana na kazi ya muziki. Kwanza, Nahreel amefanikiwa sana kutokana na ngoma kali na uwezo mkubwa alionao pamoja na mshirika wake wa kibiashara, Aika kwenye kulifanya kundi la Navy Kenzo kuwa gumzo kubwa kwa ngoma na video kali. Pili Nahreel ameweza kufanikiwa sana kwa kutengeneza BEATS ambazo zinapounganishwa na mistari mikali kutoka kwa mastaa wakali wa Bongo Fleva basi hakuna kinachofuata zaidi ya NGOMA KALI, mfano wa ngoma hizo ni DON’T

BOTHER, KAMATIA CHINI nk.

Lakini licha ya kupata pongezi nyingi bado Nahreel ameonyesha uungwana wa hal ya juu kwenye jambo ambalo huenda (kama angeliendea kwa namna tofauti) mashabiki wake wangemuunga mkono (kutokana na historia ya kazi alizokwishafanya hadi sasa) lakini huenda mwishowe lingeweza kumharibia sana.

Hivi sasa kwenye Bongo Fleva moja ya nyimbo zinazokimbiza kwenye HIP HOP ni AROSTO ya rapa G-NAKO wa kundi la WEUSI na tetesi zikawa zimeanza kuzagaa kuwa BEAR za ngoma hiyo zimetengenezwa na Nahreel huku ikifahamika kuwa beat hizo ni mali ya SWITCH RECORDS, alipoulizwa Nahreel alisema nini?

‘Siwezi kuthibitisha juu ya hilo kwa sasa, kwasababu niliwahi kutengeneza beats kama mia sita (600) nikiwa SWITCH Records kabla ya kuhama na niliiacha external drive (kifaa cha kuhifadhia kumbukumbu/nyaraka za kielektroniki) yangu kwenye studio ile hivyo sina ushahidi wa moja kwa moja juu ya umiliki wa beat hiyo’.

Je, Nahreel angedai kuwa beat hiyo ni moja ya kazi alizozifanya na kuiacha SWITCH Records miaka kadhaa iliyopita (bila ya kuwa na uthibitisho) ingekuwaje?

Yangeanza mabishano (na huenda mengi yangefanyikia kwenye social media) ambapo badala ya kupatikana kwa ufumbuzi huenda tatizo lingekuwa kubwa zaidi.

Ahsante Nahreel kwa kauli fupi iliyojaa busara ya kuepuka mgogoro usio na msingi, kama beat hiyo itakuwa ni haki yako basi utakipata kile unachostahili na kama kazi hiyo hukuitengeneza wewe basi aliyeitengeneza atapata anachostahili.

Mashabiki weu tusiwe chanzo cha ugomvi…..Ahsante Nahreel, wewe ni STAA!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *