Shirikisho la soka nchini TFF limezitaka vilabu vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara na ligi daraja la kwanza kukamilisha usajili wa wachezaji wao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu kwasababu muda uliopangwa hautasogezwa mbele.

Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa shirikisho hilo, Alfred Lucas amesema klabu zote zikamilishe usajili wake kwa wakati na zisitarajie kama muda utaongezwa kama ilivyozoeleka.

Msemaji huyo amesema kwamba uamuzi huo unatokana na muda kutoruhusu kupangua kalenda yake na kuwakumbusha viongozi wa vilabu hivyo kusajili kwa kutumia mtandao (TMS).

Dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Agosti 6 kabla ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara kuanza ifikapo Agosti 20 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *