Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga SC dhidi ya Simba siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Taarifa kutoka shirikisho imebainisha kuwa watazamaji watakaotaka kuketi kwenye jukwaa kuu watapaswa kulipia shilingi elfu ishirini 20000 ili kuona mchezo huo.

Watazamaji watakaoketi eneo la mzunguko watalipia shilingi elfu kumi, 10000 ili kushuhudia mchezo huo.

Yanga na Simba zitaingia uwanjani zote zikiwa na alama 15, Simba ikiwa juu kwa tofauti ya mabao hivyo mshindi wa mchezo huo ana nafasi kubwa ya kuongoza ligi huku akisubiri matokeo ya Mtibwa Sugar dhidi ya Singida United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *