Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kumfutia kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka wakili Damas Ndumaro ambaye alifungiwa kwa muda wa miaka saba.
Maamuzi hayo yamechukuliwa na Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Rahim Shaban Zuberi ambaye ndiye aliyetangaza maamuzi hayo kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam, leo Jumatano.
Hadi anafikia hatua ya kufunguliwa, Ndumbaro alikuwa ametumikia adhabu yake kwa muda wa miaka miwili na nusu.
Katika maelezo yake, Zuberi amesema Ndumbaro hakupata nafasi ya kujitetea na kuna badhi ya mambo hayakuzingatia usawa wakati akifungiwa.