Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanya marekebisho katika Ngao ya Jamii ambayo ilikosewa kuandikwa baada ya kuchanganya herufi kwenye maneno ya ngao hiyo.

Ngao hiyo ilitolewa kwa timu ya Simba baada ya kuifunga Yanga Jumatano iliyopita kwenye mechi ya Ngao ya Jamii katika uwanja wa Taifa.

Awali Ngao hiyo ilikosewa katika neno SHIELD, Simba walikabidhiwa lakini baada ya makosa kuonekana, TFF waliomba radhi kesho yake kisha kuwaambia Simba wairejeshe Ngao hiyo kwa ajili ya marekebisho ya neno hilo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ameionyesha Ngao iliyorekebishwa kwa waandishi wa habari leo Jumanne kwenye ofisi za shirikisho hilo, Karume jijini Dar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *