Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa (TFDA), Hiiti Sillo amewatoa wasiwasi wananchi wa Tanzania kwa kuwaambia mpaka sasa hawajapokea taarifa yeyote ya kuonesha kuwa kuna mchele wa plastiki katika masoko makubwa na madogo ya mchele.
Siilo amebainisha hayo baada ya kuenea kwa uvumi katika mitandano ya kijamii ambao ulikuwa unasambaza taarifa za kuingizwa mchele feki wa plastiki katika masoko ya mchele pamoja na maduka ya reja reja
Pia amesema kuwa “TFDA imesajili mchele wa Basmati lakini siyo huo wa brand ya sunrice, ambao taarifa zake zimekuwa zikisambaa kwa madai ni mchele wa plastiki. hatuutambui na taarifa ile sisi tulipoipokea tulianza kufanya ukaguzi wa ufuatiliaji na kiuchunguzi, mchele tunaoufahamu ni ambao umelimwa mashambani umevunwa na ndiyo ambao tunautumia kwa hiyo hatujawahi kuona mchele unaotokana na plastiki kitaalamu hatujawahi kuufahamu”.
Pamoja na hayo Sillo amewataka wananchi wawe majasiri katika kutoa taarifa za ukweli kuhusiana na tatizo hilo ili ziweze kuchukuliwa kwa haraka zisije kuathiri afya za watu.
Amesema kuwa Tuwe wajasiri tusioneshe mikono pekee yake kwa sababu tutakuwa hatujawasaidia watu bado, unalalamika kuwa umekula chakula ambacho unahisi siyo bora lakini namna ambavyo ujumbe unatufikia haujatusaidia bado tunawaomba sana wananchi watupe taarifa, sisi tumejipanga na tutawafikia hao.