Klabu ya Chelsea wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kwa pauni milioni 35 kabla ya dirisha la usajili kufungwa Alhamisi ijayo.

Chelsea wananajaribu kufanikisha usajili wa pauni milioni 15 wa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, ambaye alicheza chini ya Antonio Conte, Juventus.

Manchester City wamekata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 18, kwa pauni milioni 150.

Manchester City watapanda dau la tatu la zaidi ya pauni milioni 25 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29.

Mchezaji wa Monaco Thomas Lemar amesema angependa zaidi kujiunga na Manchester United badala ya Arsenal.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Gary Cahill alijiunga na Chelsea mwaka 2012 akitokea Bolton.

Zlatan Ibrahimovic amekubali kupunguziwa mshahara wake kwa asilimia hamsini mwezi Januari, baada ya kusaini tena kubakia Old Trafford.

Barcelona wamekubaliana mkataba wa pauni milioni 138 na Borussia Dortmund wa kumsajili mshambuliaji Ousmane Dembele, 20.

Barcelona wamesema kiungo Arda Turan, 30, anaruhusiwa kuondoka kwa uhamisho usio na malipo yoyote.

Wakala wa Julian Draxler wa PSG wamekwenda Ujerumani kuzungumza na Bayern Munich kuhusiana na uhamisho wake. (L’Equipe)

Swansea wamepuguza kasi ya kutaka kumsajili kiungo wa West Brom Nacer Chadli, 28, baada ya kuambiwa walipe zaidi ya pauni milioni na Crystal Palace wanataka kumsajili kipa wa Tottenham Michel Vorm.

Crystal Palace pia wanataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Munir El Haddadi, 21.

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Pepe Reina

Winga wa RB Leipzig Oliver Burke, 20, anakaribia kufanya vipimo vya afya kujiunga na West Brom.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *