Klabu ya Tottenham hawapo tayari kupokea dau lolote kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Danny Rose, 27, huku Chelsea wakiwa tayari kumlipa mshahara mara dufu beki huyo.

Manchester United hawana mpango tena wa kumfuatilia Danny Rose, 27, huku beki huyo akitaka kwenda Old Trafford.

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesema kiungo Dele Alli, 21, hauzwi hata kwa pauni milioni 150, huku Barcelona na Manchester City wakimfuatilia.

Tottenham wamezidiwa kete na Lyon katika kumsajili kiungo wa Celta Vigo Pape Cheikh Diop, 20. Spurs walipanda dau la pauni milioni 9.

Chelsea hawajakata tamaa ya kumsajili Alex Sandro, 26, kutoka Juventus, lakini matumaini yao yapo kwenye mchezaji huyo kuwasilisha mwenyewe maombi ya kuondoka.

Chelsea wamepanda dau la pauni milioni 73 kumtaka Alex Sandro, lakini Juventus wamekataa.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kutoa pauni milioni 25 pamoja na marupurupu zaidi ili kumsajili Danny Drinkwater, 27, lakini Leicester wanataka pauni milioni 40.

Barcelona wamewapa Liverpool pauni milioni 118 kutaka kumsajili Philippe Coutinho ili kuziba pengo la Neymar.

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa Ousmane Dembele, 20, kutoka Borussia Dortmund.

Manchester City wamepanda dau la pauni milioni 60 kumtaka Alexis Sanchez, 28, wa Arsenal. Real Madrid pia wanamtaka Sanchez.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemuambia Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kuwa anataka abakie Emirates “kwa muda mrefu” huku Chelsea, Liverpool na Manchester United wakimtaka winga huyo

Arsene Wenger amesema Alexis Sanchez, na Alex Oxlade-Chamberail huenda wakauzwa msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *