Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemwambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake kurejea Manchester United (Sun).

Manchester United watawapa Real Madrid David de Gea, 26, pamoja na pauni milioni 183, ili kumsajili Cristiano Ronaldo, 32 pamoja na Alvaro Morata, 24 (Tuttosport).

Manchester United itawapa Real Madrid David de Gea pamoja na pauni milioni 175 kumchukua Ronaldo, na pia watamfuatilia Alvaro Morata katika mkataba mwingine tofauti (Daily Mirror).

Iwapo De Gea atakwenda Real Madrid, Manchester United watamfuatilia kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma, 18 (Calciomercato)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho hamtaki Ronaldo kwa sababu anahisi kiwango chake kimeanza kushuka (Diario Gol).

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amempigia simu Ronaldo kujaribu kumshawishi asiondoke Madrid (Marca).

AC Milan huenda wakaamua kumfuatilia kipa wa Manchester City Joe Hart, 30, iwapo kipa wao Donnarumma ataondoka (Daily Express).

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amekuwa akivutia timu mbalimbali nchini Spain, Italia, Uturuki na Marekani pamoja na China, lakini Rooney pia huenda akaamua kubakia Old Trafford (Times).

Chelsea wataongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Juventus Alex Sandro, 26, pamoja na kiungo Tiemoue Bakayoko, 22 (Guardian).

Kiungo wa Italy Marco Verratti, 24, anataka kuondoka Paris Saint Germain kwenda Barcelona (Gazzetta dello Sport).

Liverpool bado wapo kwenye mazungumzo na Roma kuhusu uhamisho wa winga Mohamed Salah, 25, lakini hawataki kulipa pauni milioni 35 wanazotaka klabu hiyo ya Seria A (Sky Sports).

Everton watafikisha pauni milioni 60 za usajili wiki hii watakapokamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Malaga, Sandro Ramirez, 21 (Daily Star).

Southampton wanataka kumsajili beki wa kimataifa wa Austria, Kevin Wimmer, 24, lakini wanataka Tottenham kupunguza bei ya pauni milioni 20 (Daily Mirror).

Leicester City wanafikiria kutoa dau la pili kumtaka beki Jonny Evans, 29 kutoka West Brom (Daily Telegraph).

Chelsea wanataka kuongeza dau kufikia pauni milioni 60 kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (Daily Express).

Manchester United wamempa ‘ofa’ya mkataba mkubwa zaidi Blaise Matuidi, kuliko aliokuwa nao sasa PSG (PSG United).

Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 44 kumsajili winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins (A Bola).

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang huenda akaungana na meneja wake wa zamani Jurgen Klopp, Liverpool (Le Parisien).

Barcelona watatumia kifungu cha kumnunua tena Gerard Deulefeu kwa kutoa pauni milioni 10.5 kwa Everton (Times).

Marco Asensio huenda akaomba kuondoka Real Madrid iwapo timu hiyo itasajili wachezaji watakaomuweka ‘benchi’, huku Arsenal, Liverpool na Juventus wakiwa wamemuuliza kiungo huyo mshambuliaji (Diario Gol).

Arsenal wanajiandaa kutoa pauni milioni 26.3 kumsajili kiungo wa Barcelona Arda Turan (AMK).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *