Klabu ya Liverpool wamemuulizia kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, na wapo tayari kuvunja rekodi ya uhamisho ya klabu kwa kutoa pauni milioni 55.

Paris Saint-Germain wamefikia makubaliano ya kumsajili kwa mkopo kwanza, mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na kuweza kukamilisha usajili wa pauni milioni 166 msimu ujao.

Manchester United wamewapa Real Madrid pauni milioni 92 kutaka kumsajili Gareth Bale baada ya klabu hiyo kuonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.

Barcelona wanamuona Marcus Rashford wa Manchester United kama mrithi wa baadaye wa Luis Suarez.

Chelsea wana uhakika wa kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 30 wa kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Manchester City wapo tayari kuwapa Arsenal pauni milioni 70 pamoja na beki Jason Denayer, ili kumsajili Alexis Sanchez, 28.

Manchester City wanajiandaa kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick Aubameyang, iwapo watashindwa kumsajili Alexis Sanchez.

Leicester City wamepanda dau la pauni milioni 23 kutaka kumsajili beki wa West Brom Jonny Evans, 29.

Meneja wa West Ham Slaven Bilic anapambana vikali kulinda kazi yake baada ya kupoteza mechi tatu za mwanzo za EPL.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema yuko tayari kumruhusu Divock Origi, 22, kuondoka kwa mkopo iwapo klabu yake itaongeza wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 25, anajiandaa kuondoka Emirates na kwenda Inter Milan, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 35 kutoka Valencia.

Stoke City wamefikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili beki Kevin Wimmer, 24, kwa pauni milioni 15.

Mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, 30, ananyatiwa na Las Palmas ya Uhispania na Calgiari ya Italia.

Meneja wa Chelsea atabakia Stamford Bridge hata kama watashindwa kuongeza wachezaji wengine wapya.

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, wakilenga kusajili wachezaji watatu wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

West Brom wamepanda dau la pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Fenerbahce Josef de Souza, 28, na pia wamemuulizia beki wa Bournemouth Tyrone Mings, 24.

Swansea watapanda dau la pauni milioni 13 kutaka kumsajili tena mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, aliouzwa kwenda City kutoka Swansea mwaka 2015 kwa pauni milioni 28.

Birmingham City wanazungumza na kiungo wa kimataifa wa Ghana Afiriye Acquah, 25, kutaka kumsajili kutoka Torino.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *