Klabu ya Liverpool wamekubali kumuuza kiungo Philippe Coutinho kwenda Barcelona kwa pauni milioni 148.

Jose Mourinho anataka kumsajili winga wa Leicester City Riyad Mahrez ili kuimarisha kikosi chake.

Arsenal huenda wakashawishiwa kumuuza Alexis Sanchez, 28, iwapo watapata dau la kuvutia.

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 30 kutoka Liverpool la kumtaka Alex Oxlade-Chamberlain, ambaye pia amekataa kwenda Chelsea kwa pauni milioni 40.

Raheem Sterling atabakia Manchester City na hatokuwa sehemu ya mkataba wa City kumsajili Alexis Sanchez kutoka Arsenal.

Sergio Aguero huenda akataka kuondoka Manchester City mwezi Januari iwapo Pep Guardiola ataendelea kutomtumia.

Tottenham wanafikiria kutopanda dau la kutaka kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, kwa sababu ni majeruhi kwa sasa.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa huenda akashangaza wengi na kujiunga na Las Palmas kwa mkopo huku akisubiri kujiunga na Atletico Madrid.

Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, atakataa kujiunga na Arsenal na badala yake anataka kwenda Manchester City.

West Brom wanatarajia kumsajili beki wa kati Grzegorz Krychowiak, 27, kutoka Paris Saint-Germain.

West Brom pia wanatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Arsenal Kieran Gibbs, 27, katika saa 24 zijazo.

Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, bado ana matumaini ya kwenda Liverpool ingawa Arsenal na Chelsea huenda nazo zikapanda dau katika saa za mwisho kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Crystal Palace watamuunga mkono meneja wake Frank de Boer kwa kusajili wachezaji watatu wapya.

Stoke City wanataka kumsajili kiungo wa Manchester City Fabian Delph, 27, na wapo tayari kutoa pauni milioni 12, kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 8 kutoka Aston Villa miaka miwili iliyopita.

Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez yuko tayari kumuuza mshambuliaji wake Dwight Gayle, 26, kwa pauni milioni 18.

Winga Adama Traore, 21, anataka kuondoka Middlesbrough kwenda Lille na Divock Origi huenda akaondoka Liverpool na kwenda Tottenham, kwa mujibu wa baba yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *