Klabu ya Barcelona inatarajia kumsajili mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe kwa ajili ya kwenda kuziba pengo la Neymar  anayeeleka PSG msimu huu.

Ligi ya Uhispania haitokubali kupokea malipo ya kutengua kifungu cha uhamisho cha Neymar kutoka PSG kwa sababu ya mzozo wa malipo ya uzalendo kati ya Neymar na Barca na pia wasiwasi kuhusu PSG kukiuka kanuni za fedha za UEFA.

Barcelona hawatojaribu kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoinne Griezmann, 26, licha ya Neymar kuonekana kuwa anaondoka.

Barcelona wataziba pengo la Neymar kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele, 20, anayechezea Borussia Dortmund.

Wakala wa zamani wa Neymar Wagner Ribeiro amesema “PSG watalipa kitita cha kutengua kifungu cha usajili” wa mchezaji huyo wa Brazil na kuwa “Neymar atatambulishwa rasmi kwa mashabiki wiki hii”.

Barcelona watatumia fedha za mauzo ya Neymar kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, na Philippe Coutinho wa Liverpool.

Manchester United wapo tayari kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza kiungo chipukizi Scott McTominay, 20.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema atakuwa “mwenye furaha” iwapo timu yake itaweza kusajili mchezaji mwingine tena.

Jose Mourinho amesema mshambuliaji Anthony Martial, 21, haondoki Manchester United licha ya kuhusishwa na kuhamia Inter Milan.

Meneja wa Man Utd Jose Mourinho angependa kusajili wachezaji wengine watatu kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hata hivyo United inaarifiwa wamekata tamaa ya kumsajili winga wa Inter Milan, Ivan Perisic.

Meneja wa Tottenham anataka kumfanya kipa Paulo Gazzaniga, 25, kuwa usajili wake wa kwanza kwa kutoa pauni milioni 2 kwa Southampton.

Meneja wa Atletico Madrid Diego Simione ameiambia bodi ya klabu yake kuwa lazima wamsajili Diego Costa, 28, ambaye Chelsea wanasema anauzwa kwa pauni milioni 50.

Image caption Chelsea yasema haina haraka kumuu za Diego Costa

Chelsea hawana haraka ya kumuuza Diego Costa, na wamedhamiria kushikilia bei ya pauni milioni 50.

Chelsea wanatazamia kumsajili kiungo wa Leicester Danny Drinkwater, 27, badala ya Renato Sanches, 19 wa Bayern Munich.

Uhamisho wa pauni milioni 50 wa kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, kutoka Swansea kwenda Everton unatarajiwa kukamilika siku chache zijazo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *