Klabu ya Manchester City imesema kuwa wapo tayari kuvunja rekodi ya dunia kwa kutoa pauni milioni 275 na kutengua kipengele cha ada ya uhamisho cha Lionel Messi wa Barcelona.

Maafisa wa Manchester City wamekutana na wawakilisji wa Lionel Messi, 30, kujadili uwezekano wa mshambuliaji huyo wa Barcelona kuhamia Etihad.

Arsenal wamempa Alex Oxlade Chamberlain, 24, mkataba wa miaka minne na mshahara wa pauni 125,000 kwa wiki ili kuzuia Chelsea kumchukua.

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta, 33, ambaye mkataba wake unaisha mwakani amesema hana uhakika wa kubakia na timu hiyo.

Barcelona wapo tayari kulipa pauni milioni 36 ili kumsajili kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 26, wakiwa na matumaini kuwa atacheza na Philippe Coutinho msimu ujao.

Chelsea na AC Milan wanafuatilia mwenendo wa Pierre Emerick-Aubameyang, baada ya mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund kusema anahitaji kuondoka ili aweze kukua kisoka.

Antalyaspor ya Uturuki imempa Samir Nasri mkataba wa miaka miwili na mshahara wa pauni 70,000 kwa wiki ili kumsajili kutoka Manchester City.

Meneja wa Crystal Palace Frank de Boer amesema bei ya beki wa Liverpool Mamadou Sakho, 27, ni kubwa mno.

Manchester United wanatarajia Zlatan Ibrahimovic atasaini mkataba mpya wa kubakia Old Trafford wiki hii.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema lazima auze wachezaji kwanza kabla ya kununua wengine kwa sababu timu hiyo ina “wachezaji wengi mno”.

Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke ameituhumu Barcelona kwa kutokuwa na utaratibu mzuri katika kutaka kumsajili Ousmane Dembele.

Wachezaji wa Leicester wamemwambia Riyad Mahrez, 26, anayetaka kuondoka, abakie na klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *