Manchester United wanataka kumsajili beki wa kulia wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, 24, ambaye kwa sasa amepigwa marufuku kuingia Uingereza.

Manchester United wamemuulizia kiungo wa Anderlecht Leander Dendoncker, 22, lakini hawatarajii kumsajili msimu huu.

Monaco wamepandisha bei ya Kylian Mbappe hadi euro milioni 200 kwa matumaini kuwa Barcelona huenda wakamtaka ili kuziba pengo la Neymar anayedhaniwa kwenda PSG.

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema alizungumza na mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata kuhusu kwenda White Hart Lane, lakini Morata hakutaka kugombania namba na Harry Kane.

Arsene Wenger amemuambia mshambuliaji Alexis Sanchez, 28, kuwa hatouzwa kwa klabu yoyote ya England msimu huu.

Alexis Sanchez amewashawishi wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka Arsenal msimu huu, huku Manchester City na PSG zikiendelea kumnyatia, na kikosi cha Arsenal sasa kinaamini kweli Sanchez anataka kuondoka.

Liverpool hawamtaki Rafinha au Andre Gomes ambao wametajwa kuwa katika sehemu ya mkataba wa Barcelona wa kumtaka Philippe Coutinho.

Mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20, anafanya vipimo vya afya ili kujiunga na Leicester City kwa pauni milioni 25.

Mshambuliaji wa Valencia Alvaro Negredo, 31, anakaribia kusaini mkataba kujiunga na Besitkas, licha ya Swansea na Leeds kumtaka.

Kipa wa Arsenal David Ospina, 28, anapanga kubakia Emirates na kuipigania namba yake. Barcelona wanataka kumchukua mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, au Paulo Dybala wa Juventus kuziba pengo la Neymar.

Barcelona watataka kiungo mmojawapo wa PSG – Angel Di Maria, Julian Dexter, Adrien Rabiot au Marco Verratti kuwa sehemu ya mkataba wa kumchukua Neymar.

Image caption Barcelona wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26, kuziba pengo la Neymar.

Barcelona wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26, kuziba pengo la Neymar.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *