Chelsea wanataka kumaliza mzozo kati ya Conte na Costa, na Costa akiwa tayari kufanya hivyo ili kufahamu mustakabali wake, lakini Conte hataki kabisa (Sun)

Wakati huohuo Antonio Conte ametoa masharti kadhaa, ikiwemo kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na mmiliki wa timu Roman Abramovic, kuwa na udhibiti wa kuteua makocha wasaidizi, pamoja na mikataba bora ya kifedha, ikiwa Chelsea wanataka aendelee kubakia Stamford Bridge (Daily Record).

Mazungumzo kati ya Chelsea na kipa Thibaut Courtois, 25, yamedorora kutokana na suala la mshahara. Courtois kwa sasa analipwa pauni 100,000 kwa wiki na mkataba wake unaisha miaka miwili ijayo (Times).

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anazidi kughadhabishwa na klabu hiyo kujivuta katika kufanya usajili na huenda akawa tayari kuondoka darajani (Sky Sports Italia).

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema bei ya kipa David de Gea, 26, ni pauni milioni 100, na kama Real Madrid wanamtaka, watoe pauni milioni 45 pamoja na Alvaro Morata (Daily Star).

Cristiano Ronaldo, 32, ameiambia Real Madreid kuwa anataka kuondoka Spain na kuwa habadilishi uamuzi wake huo (A Bola).

Kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, bado anasakwa na Everton, licha ya klabu hiyo kumsajili Davy Klassen kutoka Ajax (Wales Online).

Liverpool wanataka kukusanya fedha kwa kuwauza beki Mamadou Sakho, 27, kwa pauni milioni 30, beki Alberto Moreno, 24, kwa pauni milioni 12 na Lazar Markovic, 23, kwa pauni milioni 20 (Times).

Dau la pauni milioni 17.6 la Arsenal kumtaka winga Juan Cuadrado, 29, limekataliwa na Juventus. Klabu hiyo ya Italia inataka takriban pauni milioni 30 kumuuza mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea (Sun).

Arsenal wametoa pauni milioni 10.5 kumtaka beki wa kati wa Fenerbahce Simo Kjaer, 28, ambaye pia anasakwa na AC Milan na Inter Milan (Turksvoetbal).

Winga wa Inyter Milan Ivan Perisic, 28, tayari anajiandaa kuwa mchezaji wa Manchester United, ingawa timu hizo mbili bado hazijafikia makubaliano ya pauni milioni 44 za uhamisho (Manchester Evening News).

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Alvaro Morata huenda akakamilisha kuhamia Manchester United

Real Madrid wanasisitiza kuwa wanataka pauni milioni 78 kumuuza Alvaro Morata, 24, licha ya taarifa za kupewa ‘mkataba mnono’ na Manchester United (Independent).

Baada ya kukamilisha usajili wa beki Victor Lindelof, Manchester United huenda wakarejea Benfica kumsajili kiungo Anderson Talisca, 23, kwa pauni milioni 15. Talisca alicheza kwa mkopo Besitkas msimu uliopita (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Manchester City Patrick Roberts, 20, aliyefunga mabao 11 msimu uliopita akiichezea Celtic, anazungumza na Nice ya Ufaransa kwa ajili ya kwenda kwa mkopo (Sun).

Tottenham ni moja ya timu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Lazio, Keita Balde, 22, ambaye ana thamani ya pauni milioni 30 (Daily Mirror).

Southampton wanataka kumfanyia usaili meneja wa zamani wa Ajax, Frank de Boer na pia meneja wa zamani wa Valencia Mauricio Pellegrino, kuziba nafasi ya Claude Puel, na wana matumaini ya kutangaza meneja mpya mwishoni mwa wiki ijayo (Daily Telegraph).

Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel amesema hawanii nafasi ya kazi ya Southampton (Sky Sports).

Stoke huenda wakataka zaidi ya pauni milioni 30, iwapo watamuuza kipa Jack Butland, 24, ingawa wamesisitiza kuwa hauzwi (Stoke Sentinel).

Timu kadhaa za EPL ikiwemo Newcastle United zinamuulizia beki wa kati wa Valencia Aymen Abdennour, 27, kwa pauni milioni 13.1 (Foot Mercato).

Paris Saint Germain wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick Aubameyang, 27, kwa sababu bei ya pauni milioni 61 ni kubwa mno, kwa mujibu wa mkurugenzi wa michezo wa PSG Antero Henrique (Goal.com).

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameanza mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid Toni Kroos (Don Balon).

Real Madrid wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili Gianluigi Donnarumma kutoka AC Milan, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Paris Saint Germain (Sky Sports Italia).

Arsenal wako tayari kumtumia Olivier Giroud kama chambo ili kumsajili Kylian Mbappe au Alexandre Lacazette (Daily Express).

Southampton wanataka kumsajili Ben Gibson ili kuziba nafasi ya Virgil van Dijk (Daily Mirror).

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *