Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, ana wasiwasi kuwa huenda Arsenal wakazuia uhamisho wake kwenda Manchester City, na hivyo kuacha Bayern Munich kuwa kimbilio pekee (Mirror).

Arsenal wametakiwa kulipa pauni milioni 55 na pauni milioni 12 za ziada iwapo wanataka kumsajili mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 26 (Daily Telegraph) nao Aston Villa wanataka kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36 (Sky Sports).

Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoinne Griezmann, 26, amesaini mkataba kusalia Madrid hadi mwaka 2022, (AS) naye mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 35, ameanza mazungumzo kuhusu kuhamia LA Galaxy ya Marekani (Yahoo).

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, naye amesema tetesi zinazomhusisha yeye kuhamia Barcelona ‘sio suala jepesi’ (Independent), mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anajiandaa kuondoka kwa mkopo ili kufanikisha uhamisho wake kwenda Atletico Madrid (Evening Standard).

Meneja wa Chelsea amemuambia Cecs Fabregas, 30, kuwa atakuwa katika kikosi chake msimu ujao, huku Nemanja Matic, 28, akiwa na uwezekano mkubwa wa kuuzwa (Daily Express).

Chelsea huenda wakapanda dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, 26, iwapo Eden Hazard atakwenda Real Madrid (Sun).

Manchester City wanajiandaa kuanza mazungumzo na Tottenham kuhusu usajili wa beki Kyle Walker, 27 (Sky Sports), Alvaro Morata anakaribia kujiunga na Manchester United baada ya wakala wa mchezaji huyo kusema haendi AC Milan (Mirror),.

Juventus wanataka kumsajili winga kutoka Algeria Riyad Mahrez, 26, anayechezea Leicester City.

Tottenham nao wanamtaka mshambuliaji wa Leicester Demarai Gray, 20 (Mirror), mshambuliaji wa Croatia na Inter Milan Ivan Perisic, 28, amesema anataka kuhamia Manchester United (Corriere Dello Sport), winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22, anasakwa na Real Sociedad ya Spain kwa pauni milioni 8.8 (TalkSport).

Mshambuliaji wa Newcastle Aleksandar Mitrovic, 22, amekiri kuwa huenda akaondoka msimu huu iwapo dau zuri litatolewa, na Fenerbahce wamehusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia (Daily Star).

PSG wamesema kiungo wao Marco Verratti, ambaye anasakwa na Barcelona, hauzwi (Marca), Real Madrid wanatazamiwa kukamilisha uhamisho wa Kylian Mbappe na kumrejesha Monaco kwa mkopo (AS).

Manchester United wamekubaliana ‘kimsingi’ kumsajili James Rodriguez, lakini mkataba wake na Adidas unamtaka avae jezi namba 10 anayovaa Wayne Rooney ambaye hatma yake Old Trafford bado haijulikani (OK Diario).

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Terry aliisaidia Chelsea kushinda vikombe vitano vya FA, Vitatu vya Ligi ya EPL, kombe la mabingwa Ulaya mara moja na Europa ligi mara moja.

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches atawatosa Manchester United na kusubiri dau kutoka Barcelona (Daily Mail), meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amewasiliana na wakala wa Kylian Mbappe ili kujitosa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 100 (Daily Mail).

Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa winga kutoka Roma Mohamed Salah (Corriere dello Sport), Barcelona watatoa euro milioni 100 kumtaka Marco Verratti (La Gazzetta dello Sport), huku Bayern Munich wakikaribia kukubaliana ada ya uhamisho na kiungo wa Lyon Corentin Tolisso (Kicker). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *