Paris Saint-Germain wanataka kuwapiku Manchester City katika dakika za mwisho na kumsajili Dani Alves.

Beki huyo kutoka Brazil alionekana kukaribia kuhamia City lakini PSG huenda wakamchukua (Le10Sport).

Wakala wa James Rodriguez amewaambia Liverpool, Manchester United, Inter Milan, Juventus, Manchester City na PSG kuwa wanaweza kumsajili kiungo huyo wa Real Madrid, lakini hakuna kati ya timu hizo iko tayari kutoa euro milioni 75 wanazotaka Real, ambao wanataka kumuuza kutokana na kuwasili kwa Dani Caballos (SPORT).

Beki wa Southampton Virgil van Dijk ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Liverpool tu (Mirror).

Manchester United wapo tayari kuwapiga kumbo jingine Chelsea kwa kumsajili James Rodriguez. Chelsea na PSG zinamtaka mchezaji huyo lakini James mwenyewe angependa kwenda kwa Mourinho (Express).

Baada ya kuwazidi kete Chelsea katika kumsajili Romelu Lukaku, Manchester United wamemsajili Lomelu Lukakuwanataka kuwapiku tena katika kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco, ambao wamekasirishwa na kasi ndogo ya Chelsea kumfuatilia mchezaji huyo. United watamchukua ikiwa watashindwa kumpata Nemanja Matic kutoka Chelsea (The Sun).

James Rodrigues anataka kuhakikisha anaondoka Real Madrid katika saa 48 zijazo ili asisafiri na Real Madrid kwenda Marekani katika mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (AS).

Arsenal wamekubaliana maslahi binafsi na Thomas Lemar ya mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, lakini bado hawajafikia makubaliano na Monaco (the Sun).

Celta Vigo wanafikiria kumchukua winga wa Borussia Dortmund Emre Mor ambaye pia amehusishwa na Liverpool (Atlantico).

Dani Ceballos, 20, amekubali mkataba wa miaka sita kujiunga na Real Madrid kutoka Real Betis na atakamilisha mkataba wa euro milioni 18. Barcelona walikuwa ‘wakimchombeza’ mchezaji huyo (Marca).

Antonio Rudiger anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma kwenda Chelsea kwa pauni milioni 34 na mkataba utakamilika katika saa 24-48 zijazo (Sky).

Arsenal wameweka wazi kuwa hawatomuuza Alexis Sanchez au Alex Oxlade- Chamberlain kwenda katika timu yoyote hasimu ya EPL. Sanchez ananyatiwa na Manchester City huku Oxlade-Chamberlain akihusishwa na Liverpool (Daily Star).

Arsenal watakuwa tayari kumuuza Alexis Sanchez kwenda Manchester City ikiwa tu watatoa pauni milioni 80 (Mirror).

Arsenal wameongeza dau lao hadi pauni milioni 40 kutaka kumsajili winga Thomas Lemar, 21 kutoka Monaco, baada ya pauni milioni 35 za awali kukataliwa (L’Equipe).

Meneja Antonio Conte atarejea Chelsea siku ya Jumatatu kutoka likizo na kutaka mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kushindwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton (Express).

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, 31, amefanya vipimo vya afya Everton (Sky Sports).

Zlatan Ibrahimovic, 35, huenda akapewa mkataba mpya na Manchester United baada ya kupona jeraha la goti (Mirror).

Tottenham wamesema kiungo wao Eric Dier, 23, hauzwi kwa bei yoyote. Hii ni baada ya kuhusishwa na Manchester United kwa pauni milioni 50 (Mail).

Jose Mourinho ameongeza juhudi za majadiliano kutaka kumsajili James Rodriguez, 25, kutoka Real Madrid. Real wanataka pauni milioni 62 (Independent).

Newcastle wamekuwa na mazungumzo na Middlesbrough ya kutaka kumsajili winga Adama Traore, 21 ambaye huenda akagharimu hadi pauni milioni 20 (Chronicle).

Newcastle wapo tayari kulipa euro milioni 20 kumsajili Andreas Samaris kutoka Benfica (O Jogo).

Kiungo wa Bayern Munich Douglas Costa anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Juventus na huenda akahamia moja kwa moja baadaye kwa euro milioni 40 (La Stampa).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *