Kiungo wa timu hya Taifa ya Uingereza, Eric Dier anataka kuondoka Tottenham ili kujiunga na Manchester United ambao wanatarajiwa kutoa dau la pauni milioni 50.

West Brom wanataka kuwasajili Chris Smalling na Phil Jones kutoka Manchester United. (Daily Mirror)

Winga wa Manchester United Adnan Januzaj anakaribia kujiunga na Real Sicieada kwa pauni milioni 9.8. (Daily Telegraph)

Manchester United wanatakiwa kutoa pauni milioni 9 zaidi ili kuweza kufanikisha usajili wa Ivan Perisic, ambapo huenda Old Trafford wakatoa pauni milioni 50. (The Telegraph)

Manchester United watampa Zlatan Ibrahimovic mkataba wa muda mfupi atakapopona jeraha la goti. (The Sun)

Manchester United hawana mpango wowote wa ‘kumnyakua’ kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko ambaye anakaribia kwenda Chelsea. (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alikutana na Kylian Mbappe, 18, Juni 14 mjini Paris kujaribu kumshawishi ahamie Emirates. (France Football)

Meneja wa PSG Unay Emery alikutana na wawakilishi wa Klylian Mbappe wiki iliyopita kujaribu kumshawishi mchezaji huyo wa Monaco kwenda Paris. (L’Equipe)

Chelsea wanataka kuwapiki Atletico Madrid katika kumsajili winga wa Sevilla Vitolo. (Cadena Cope)

Lucas Leiva huenda anaelekea Lazio baada ya kutopewa mkataba mpya na Liverpool. (Daily Star)

Atletico Madrid wanataka sana kumsajili Diego Costa, baada ya kushindwa kuwapata wachezaji watatu iliyokuwa ikiwanyatia.

Pia Atletico wanamtaka Fabinho kutoka Monaco. (independent)

PSG wanafikiria kumchukua beki wa kati wa Manchester City Eliaquim Mangala, 26. (ESPN)

PSG wanakaribia kumsajili beki Dani Alves, 34, licha ya kuwa Man City kumtaka. (telegraph)

Everton wanataka kuziba pengo la Romelu Lukaku kwa kumsajili Christian Benteke, ingawa Crystal Palace wamesema mshambuliaji huyo hauzwi. (Daily Mirror)

West Ham wanataka kumsajili kipa wa Man City Joe Hart, 30, lakini kwa mkopo. (Telegraph)

Marseille hawajakata tama ya kufikia makubaliano na Tottenham ya kumsajili Moussa Sissoko, 27. (Evening Standard)

West Brom ni miongoni mwa timu 20 zinazomwania beki wa Chelsea Kurt Zouma, 22. (Daily Mirror)

Douglas Costa, 26, amewasili mjini Turin kukamilisha uhamisho wake kwenda Juventus. (ESPN)

Manchester Uniuted wameanza mazungumzo na kiungo wao Ander Herera ya kumpa mkataba mpya wa mshahara wa pauni 175,000 kwa wiki. (Daily Star).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *