Beki wa Manchester City, Aleksander Kolarov anakaribia kujiunga na Roma, kwa mujibu wa meneja wake Pep Guardiola.

Barcelona wamewasilisha dau la pauni milioni 72 kumtaka kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, lakini Liverpool wanatarajiwa kutupilia mbali dau hilo.

Liverpool wamesema Barcelona wanapoteza muda wao kutaka kumsajili Philippe Coutinho, 25.

Arsenal wana uhakika kuwa kiungo wao Mesut Ozil, 28, atasaini mkataba mpya kubakia Emirates.

Manchester United sasa wameelekeza nguvu zao kumtaka beki wa kulia wa Paris Saint-Germain, Serge Aurier, 24, kutokana na kusuasua kwa mipango ya kumsajili Fabinho, 23, kutoka Monaco.

Meneja wa PSG Unai Emery amethibitisha kuwa Serge Aurier anataka kuondoka Paris msimu huu.

Manchester United wanataka kuwazidi kete AC Milan katika kumsajili Renato Sanches kutoka Bayern Munich.

Manchester United bado hawajafikia dau wanalotaka Inter Milan katika kumsajili Ivan Perisic, 28.

Wolfsburg wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial.

Diego Costa huenda akacheza kwa mkopo AC Milan, wakati akisubiri kuhamia Atletico Madrid.

Chelsea wapo tayari kumuuza Diego Costa kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 44, na sio pauni milioni 25 zilizotolewa na Atletico.

Alexis Sanchez, 28, amefikia makubaliano na Paris Saint-Germain, na klabu hiyo ya Ufaransa itapanda dau la pauni milioni 45. Kinachosubiriwa ni kauli ya Arsene Wenger.

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, yuko tayari kwenda West Ham, iwapo klabu hiyo itafikia makubaliano kuhusu ada ya uhamisho.

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 16, la kumsajili beki wake Callum Chambers. Arsenal wanataka pauni milioni 20.

Tottenham wametaka kufahamishwa msimamo wa Riyad Mahrez, lakini Leicester watalazimika kupunguza bei ya pauni milioni 50, kama watamuuza kwenda White Hart Lane.

Wachezaji wa Leicester City wapo tayari ‘kumhamasisha kwa lazima’ Riyad Mahrez ikiwa hatajituma kwa asilimia 100, amesema kiungo Andy King.

Meneja wa Leicester City Craig Shakespeare amethibitisha kuwa wamekataa dau kutoka Roma la kumtaka Riyad Mahrez.

Mshambuliaji wa Stoke City, Marco Arnautovic, 28, atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi West Ham baada ya kukamilisha vipimo vyake vya afya siku ya Ijumaa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *