Klabu ya Chelsea wameambiwa wanaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, kwa pauni milioni 60 baada ya Tianjin Quanjian ya China kusema haitaki tena kumsajili mchezaji huyo.

Borussia Dortmund huenda wakaamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30, ambaye pia anasakwa na Everton, West Ham, Marseille na AC Milan.

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 26, amempigia simu meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na kumuambia hana mpango wa kuondoka Chelsea msimu huu.

Chelsea wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kwa pauni milioni 40 kwa mkataba wa miaka mitano.

Meneja wa Chelsea anajiandaa kumuuza kiungo Nemanja Matic, 28, kwa pauni milioni 40. Matic amekuwa akifanya mazoezi peke yake na anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford.

Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta baada ya kushindwa kumpata Hector Bellerin wa Arsenal.

Chelsea watawazidi kete Juventus katika kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 25, kwa pauni milioni 28.

Mchezaji wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema klabu hiyo inakaribia kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton.

Arsenal wana uhakika dau la pauni milioni 45 litatosha kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar, 21.

Tottenham wamesema hawatoburuzwa na Manchester United na Manchester City kuhusu usajili wa Eric Dier na Kyle Walker, huku wakikaribia kumsajili beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes kwa pauni milioni 9.

Manchester United wana matumaini ya kukamilisha usajili wa winga wa Inter Milan Ivan Persic, 28, wiki ijayo.

Manchester United sasa wataelekeza nguvu zao kumsajili kiungo wa Roma Radja Nainggolan, 29, kwa kutoa pauni milioni 40 baada ya Tottenham kukataa dau lolote kuhusu Eric Dier.

Leicester City huenda wakaondoa wachezaji sita waliosajiliwa msimu uliopita akiwemo Islam Slimani, 29, na Ahmed Musa, 24, pamoja na kiungo Nampalys Mendy, 25.

Middlesbrough wamewazidi kete Burnley na Watford katika kumsajili Britt Assombalonga, 24, kwa pauni milioni 14 kutoka Nottingham Forest.

West Ham wanafikiria kupanda dau la tatu kumtaka Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la pauni milioni 20 kukataliwa na Stoke City.

Real Madrid wamekata tamaa ya kumpata kipa wa Manchester United David de Gea, 26, msimu huu.

Manchester City wanakaribia kumsajili kiungo kutoka Brazil Douglas Luiz, 19, anayechezea Vasco da Gama.

Manchester City wanataka kupanda dau la pauni milioni 25 kumtaka beki wa Southampton Ryan Bertrand, 27, baada ya kumkosa Dani Alves aliyesaini PSG.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *