Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda bado akahamia Liverpool kwa pauni milioni 60 msimu huu. Mchezaji huyo amesisitiza anataka tu kwenda Liverpool.

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amepigwa picha kwenye Instagram akiwa amevaa jezi ya Atletico Marid na kuandika “mpe salaam zangu Conte”.

Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya kumkosa Romelu Lukaku, 24.

Chelsea wameonywa na Borussia Dortmund kuwa wana wiki moja tu ya kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anadhani kuwa ataweza kumshawishi Alexis Sanchez, kutoondoka Emirates.

Vinginevyo Arsene Wenger anafikikia kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele, 20.

Arsene Wenger amekata tama ya kumsajili Kylian Mbappe, 18, na badala yake sasa anaelekeza nguvu katika kumsajili Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco.

Arsenal pia wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, kuziba nafasi ya Alexis Sanchez ikiwa ataondoka.

Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wa miaka mitano winga wa Atletico Madrid Yannick Carasco, 23.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka Toni Kroos, 27, kuwa sehemu ya mkataba wowote utakaomhusisha David de Gea kwenda Real Madrid.

Manchester United wanaonekana kukaribia kumpata kiungo wa Inter Milan Ivan Perisic.

Zlatan Ibrahimovic amekataa nafasi ya kujiunga na LA Galaxy na anapanga kusaini mkataba mpya na Manchester United.

Paris Saint-Germain wanapanga kutoa euro milioni 150 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio.

AC Milan wananamnyatia mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Gazzetta dello Sport)

Barcelona wapo tayari kutoa euro milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumsajili Marco Verratti kutoka PSG.

Tottenham wanataka kujaribu tena kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. Timu hizo mbili zimeshindwa kukubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji huyo.

Tottenham wana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19, mwishoni mwa wiki hii.

Loic Remy, 30, anatazamiwa kuondoka Chelsea msimu huu, huku Everton na Southampton zikimtaka.

West Ham watapanda dau la tatu kumtaka winga wa Stoke Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la awali kukataliwa.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *