Klabu ya Chelsea wanazidi kupata uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain kwa pauni milioni 35.

Chelsea wamempa masharti kadhaa Diego Costa, 28, ambayo lazima ayatimize ili waweze kumuuza.

Chelsea wanapanga kutumia pauni milioni 120 kusajili wachezaji watatu, Alex Oxlade-Chamberlain, Virgil Van Dijk na Danny Drinkwater.

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amesema atajaribu kumshawishi Philippe Coutinho, 25, asiondoke na kujiunga na Barcelona.

Borussia Dortmund wamekubali dau la euro milioni 100 kutoka kwa Barcelona ili kumsajili Ousmane Dembele, 20, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana kuhusu marupurupu.

Beki wa kati wa Southampton Virgil Van Dijk, 26, ana uwezekano mkubwa wa kuhamia Chelsea au Manchester City kuliko Liverpool, huku Southampton wakitaka zaidi ya pauni milioni 70 kumuuza mchezaji huyo.

Manchester City wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 60 kumtaka mshambuliaji wa Aresenal Alexis Sanchez.

Beki wa Ajax Davinson Sanchez, 21, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Tottenham kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Chelsea pia wanamtaka Davinson Sanchez, lakini Ajax wamesisitiza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia hauzwi.

Newcastle wanatarajia kumsajili winga wa Chelsea, Kenedy, 21, kwa mkopo, lakini Antonio Conte anasita kumuachia aondoke kwa kuwa kikosi chake kina wachezaji wachache.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *