Kocha wa Chelsea Antonio Conte atakabidhiwa pauni milioni 150 zaidi za usajili huku akitaka kumchukua Virgil van Dijk, 26, kutoka Southampton na beki wa kushoto wa Juventus, Alex Sandro.

Chelsea huenda wakatumia fedha zaidi wakati Antonio Conte akitaka kumsajili Antonio Candreva, 30, kutoka Inter Milan na pia mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32 na pia kiungo wa Everton Tom Davies, 19.

Chelsea vilevile wanataka kuwasajili Cedric Soares na Ryan Bertrand kutoka Southampton baada ya kumkosa Danilo na Benjamin Mendy.

Chelsea wapo tayari kulipa euro milioni 40 za kutengua kifungu cha usajili ili kumchukua Sergi Roberto kutoka Barcelona.

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, yuko tayari kupunguziwa mshahara ili aweze kujiunga na Manchester City. Sanchez anapenda kwenda City kuliko Bayern Munich, PSG au Juventus.

Arsenal na Liverpool huenda wakaamua kumsajili Karim Benzima, 29, iwapo Real Madrid wataamua kumuuza ili kumchukua Kylian Mbappe. Hata hivyo Real huenda wakamtumia Benzima pia kama chambo kwa Monaco ili kupunguza bei ya Mbappe.

Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kimataifa wa Poland, Sebastian Szymanski, 18, ambaye anachezea Legia Warsaw.

Liverpool wamewaambia Crystal Palace watoe pauni milioni 30 kumchukua beki Mamadou Sakho, 27, na kuwa hawatokubali kumtoa kwa mkopo tena.

Liverpool wametoa dau la pauni milioni 74 kumtaka kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22, baada dau mbili za awali kukataliwa.

Emre Can amefikia makubaliano ya maslahi binafsi na Juventus na anasubiri dau rasmi la pauni milioni 30.4 kutolewa ili kufanikisha uhamisho wake.

Manchester City wamedhamiria kufunga dirisha la usajili kwa kumwaga fedha kwa kumsajili Alexis Sanchez, 28, au Kylian Mbappe, 18. Pep Guardiola hatoridhika mpaka ampate Sanchez anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50 au Mbappe ambaye ada yake inaweza kufika pauni milioni 100.

Roma wametoa pauni milioni 30 pamoja na marupurupu mengine kumtaka Riyad Mahrez, 26, lakini Leicester wanataka pauni milioni 50.

Riyad Mahrez, 26, Huenda akajikuta amebakia Leicester msimu ujao iwapo timu zinazomtaka ikiwemo Arsenal zitashindwa kutoa pauni milioni 50 kumsajili.

Everton wana uhakika wa kukamilisha usajili wa kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, kwa pauni milioni 45, ifikapo siku ya Alhamisi.

Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 19, kwa mujibu wa meneja Carlo Ancelotti, lakini Arturo Vidal, 30, haondoki kwa mabingwa hao wa Bundesliga.

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho atakataa dau lolote la kumtaka Ashley Young, 32, ambaye Stoke City wamekuwa wakimuulizia.

Galatasaray wanazungumza na Arsenal kuhusu kumsajili kiungo kutoka Misri Mohamed Elneny, 25.

Paris Saint-Germain wamewapa Barcelona kiungo Marco Verratti pamoja na pauni milioni 90 juu, ili kumsajili Neymar.

Kiungo wa Chelsea Mason Hunt, 18, amesaini mkataba mpya wa miaka minne kabla ya kwenda Vitese kwa mkopo.

Marseille wanazungumza na Celtic kutaka kumsajili mshambuliaji Moussa Dembele, 21, kwa pauni milioni 20.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *