Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amesema kuwa huenda akastaafu baada ya jana kuwasaidia mabingwa hao wapya wa EPL kuilaza Watford kwa magoli 4-3 katika uwanja wa Stamford Bridge.
Terry mwenye miaka 36 ambaye amefunga goli la kwanza katika mchezo huo, ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Chelsea watakuwa wenyeji wa Sunderland siku ya Jumapili hii ikiwa ni mchezo wa mwisho kabisa kwa msimu huu.
Terry ameichezea Chelsea michezo 716 hii ikiwa ni tokea mwaka 1998 alipojiunga na klabu ya hiyo London.
Ameisaidia Chelsea kushinda vikombe vitano vya EPL, Vitatu vya FA, kombe la mabingwa Ulaya mara moja na Europa ligi mara 1.