Aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Tenga ameteuliwa kuwa rais wa kamati ya usimamizi wa mfumo wa leseni kwa vilabu.

Uteuzi huo umekuja muda mchache baada ya kukaa kikao cha kamati ya Utendaji chini ya uenyekiti wa CAF Rais Ahmad walipokutana hivi karibuni katika Hoteli ya Sheraton Manama, Bahra

Tenga atakuwa akisaidiwa na Rais wa Shirikisho la Soka nchini Afrika (SAFA) Kusini anayeitwa Danny Jordan.

Danny Jordan ameteuliwa kuwa makamu wa kamati hiyo pamoja na kupewa cheo kingine cha urais katika kamati ya Masoko na Televisheni.

Kuchaguliwa kwa Tenga katika nafasi hiyo kunatoa mwanga kwa soka la Tanzania kutona na viongozi wao kuchaguliwa kufanya kazi kwenye chombo kikubwa cha soka Barani Afrika (CAF).

Tenga alikuwa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kusaidia kupanda rangi kwa timu ya taifa ya Tanzania wakati wa utawala wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *