Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Mh. Temba amefunguka kwa mara ya kwanza sababu iliyofanya kundi la Yamoto Band kuvunjika.

Temba ambaye kwasasa anaisimamia kituo cha Mkubwa na Wanawe ameamua kuweka suala la kuvunjika kwa kundi hilo baada ya kukutana na maswali kila wakati.

Temba amesema majungu yaliyopikwa na watu wa nje na tamaa za kuwa na wasanii hao ambao wao wamehangaika kuwatoa kuanzia chini, ndio sababu kubwa ya kundi hilo kusambaratika.

Yamoto Band kabla ya kundi kuvunjika.
Yamoto Band kabla ya kundi kuvunjika.

Msanii huyo amesema kuwa kuna watu walikuwa wakitamani kuwasimamia wasanii hao mmoja mmoja  na sio kundi zima.

Kundi hilo kwasasa limevunjika na kila mmoja anafanya kazi peke yake kama solo artist baada ya kusambaraika ambapo baadhi yao wameshaachia nyimbo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *