Wanamuziki nyota wa Nigeria, Tekno na Yemi Alade wanatarajia kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta litakalofanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Novemba 5 mwaka huu.

Wasanii ha wametajwa kutumbuiza kwenye kilele cha tamasha la Fiesta, litakalofanyika jijini Dar kwenye viwanja vya Leaders, Novemba 5.

Nguli wa muziki kutoka Uganda, Jose Chameleone naye atatumbuiza kwenye show hiyo.

tekno-6

Wasanii wengine ndani ya Tanzania watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Alikiba, Raymond, Mr Blue, Belle 9 ba wengine.

Bado haijajulikana ni msanii yupi kutoka Marekani atakayetumbuiza mwaka huu.

Tamasha la Fiesta linatarajiwa kufikia tamati Novemba 5 mwaka huu baada ya kuzunguka mikoa mbali mbali hapa nchini.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *