Mkali wa wimbo ‘Diana’ Tekno kutoka Nigeria anatarajia sanii kuungana na wasanii kama Davido, Wizkid na Alikiba kwenye Lebo maarufu ya muziki Sony Music’.

Tekno ambaye anatarajia kutua nchini kwenye tamasha la Fiesta inawezekana akajiunga Sony Music Global hivi karibuni.

Kwa mujibu wa post aliyoweka boss wa Upfront & Personal, muanzilishi wa tamasha la One AfrikaPaul O akiwa kwenye makao makuu ya label hiyo kubwa duniani, New York amedai Tekno anasaini dili kubwa na Sony Music Global.

Iwapo Tekno atafanikiwa kusaini na Sony basi atakuwa ameungana na Davido, Wizkid, Alikiba na Ycee aliyesaini wiki chache zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *