Watoto wawili wa kitanzania wamechaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika Academy ya klabu ya Manchester City nchini Uingereza.

Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile, Eric Mkomoya amesema kuwa kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cx toleo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakini pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo.

Nao wazazi wameeleza kufaha yao kuona vijana wao amepata nafasi hiyo kwani wanaamini kuwa watoto wao watafanya vizuri katika fursa hiyo.

Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wenye umri wa miaka 12, wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile na asasi ya michezo ya Magnet, na wataondoka kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30.

Msafara huo utaongozwa na wazazi na walezi watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji vya vijana kocha Juma Maswanya.

Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa safari hiyo ambapo wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambazo ni Nigeria, Misri , Tanzania, Ghana pamoja na Kenya.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *