Shirika la viwango nchini, TBS limefungua ofisi za kanda katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kudhibiti mianya ya uingizaji wa bidhaa hafifu nchini unaofanywa na wafanyabiashara wasio waaminifu.

Kaimu mkuu wa TBS, Dr Egid Mubofu amesema ofisi hizo zitafanya kazi karibu na wazalishaji viwandani ili wananchi wapate bidhaa zenye viwango.

Hivyo amewataka viongozi wa mikoa hiyo kufichua viwanda vinavyozalisha bidhaa bila kufuata utaratibu.

Mkurugenzi huyo amesema ofisi ya Arusha itahudumia mikoa ya kanda ya kaskazini ikiwemo Manyara, Kilimanjaro, Tanga na Arusha yenyewe na ofisi ya Mwanza itahudumia kanda ya ziwa mikoa ya Mara, Kagera, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza yenyewe.

Ofisi ya Mbeya itahudumia Nyanda za Juu Kusini ya Iringa, Songwe,Ruvuma, Njombe na Mbeya yenyewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *