Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema atalifumua na kuliunda upya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa lengo la kufanya kazi kwa umakini

Waziri huyo amesema kwamba wameshaanza kutafuta vijana 136 watakaoajiriwa katika shirika hilo kwa lengo la kudhibiti bidhaa, zinazoingizwa nchini chini ya viwango.

Amesema wataweka kitengo maalumu kwa vijana hao, watakaokuwa na uwezo wa kuchunguza mipaka ya nchi, kunusanusa katika bandari bubu, kukamata, kuwasiliana na Polisi na kusimama mahakamani kutoa ushahidi.

Mwijage ameyasema hayo Dar es Salaam wakati wa utoaji wa tuzo kwa washiriki wa Programu ya Kaizen iliyo chini ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Alisema lengo la kuiunda upya TBS ni kuhakikisha kwamba kazi zinafanyika ipasavyo ili kulinda viwanda vya ndani, vinavyozalisha bidhaa mbalimbali.

Hatua yake hiyo imekuja siku chache, baada ya makontena 100 kutoroshwa katika bandari kavu za Dar es Salaam bila ya kukaguliwa na hivyo kuikosesha mapato serikali na pia kuwa na hatari ya kuingiza bidhaa zilizo chini ya kiwango.

Akizungumza utekelezaji wa agizo la Mwijage na hadi Jumanne wiki hii kwa waliotorosha makontena hayo kujisalimisha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Egid Mubofu alisema jana kuwa waziri ameongeza siku za utekelezaji wa agizo lake la kuwataka wafanyabiashara walioingiza maontena 100 bandarini bila kukaguliwa na TBS, watoe taarifa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *