Shirika la Viwango nchini (TBS) limefafanua kuwa halijaanzisha tozo mpya kwa waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dk Egid Mubofu amesema kwa kuwa siku ya mwisho ya kukaguliwa kwa kontena hizo ilikuwa jana kama ilivyotangazwa na waziri, wao watafanya kazi hadi usiku ili kuwahudumia wafanyabiashara watakaojitokeza jana kukaguliwa.

Amesema pia atawasiliana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kujua hatua zitakazochukuliwa kwa wafanyabiashara watakaoshindwa kukaguliwa ndani ya muda uliowekwa.

Mwijage ametoa siku tano kwa wafanyabiashara wanaodaiwa kutorosha kontena 100 bila kukaguliwa wahakikishe wanawasilisha kontena zao ili zikaguliwa na kujua kilichomo kwenye kontena hizo.

Ametoa msamaha kwa watakaojitokeza wasichukuliwe hatua stahiki za kisheria, bali watalazimika kulipia tozo ya asilimia 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *