Kampuni ya bia TBL kupitia kinywaji chake Kilimanjaro Lager baada ya miaka minne kuzidhamini timu za Simba na Yanga kwasasa wamesema hawataendelea kuzidhamini timu hizo kutokana na mkataba wao unafika tamati.

TBL wameamua kutoendelea kuwa wadhamini wa vilabu hiyo kutokana na Yanga kukataa kuendelea kudhaminiwa na tayari imeshapata udhamini toka kwa Quality Group Centre hivyo hawawezi kuidhamini Simba peke yake.

simba_sc-600x400

Kampuni hiyo kwa sasa watabaki kuwa wadhamini wa timu ya Taifa Star ambao bado mkataba wao haujaisha.

Kwahiyo msimu wa ligi kuu Tanzania Bara ukianza hawatakuwa wakizidhamini Simba na Yanga na wamesema wataendelea kusaidia mpira hapa nchini pamoja na kutangaza bidhaa zao.YANGANEW

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *