Mwanamuziki wa Marekani, Taylor Swift ameachana na mpenzi wake Tom Hiddleston aliyedumu naye kwa miezi mitatu tu kwenye mahusiano yao.

Wawili hao waliingia kwenye mahusiano baada ya Swift kutengana na aliyekuwa mpenzi wake aliyedumu naye kwa miezi 15, Calvin Harris.

Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa wawili hao amedai kuwa sababu ya kuvunjika kwa mahusiano hayo ni kutokana na Tom kutaka mahusiano yao kuwa wazi zaidi lakini Taylor hakutaka yawe hivyo.

Taylor Swift na aliyekuwa mpenzi wake Tom Hiddleston
Taylor Swift na aliyekuwa mpenzi wake Tom Hiddleston

Tom alikuwa ni mwanaume wa tisa kuwa na mahusiano na mwanamuziki huyo Taylor Swift wengine ni :

Joe Jonas (July 2008 – October 2008)
Lucas Till (2009)
John Mayer (August 2009 – November 2009)
Taylor Lautner (November 2009 – February 2010)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *