Mwanamuziki nyota wa Marekani, Drake amemtambulisha Taylor Swift kwa mama yake pamoja na watu wake wa karibu zikiwa ni ishara za awali za kuonyesha mahusiano yao.

Drake alifanya hivyo kwenye sherehe yake ya kutimiza umri wa miaka 30 iliyofanyika Los Angeles nchini Marekani.

Kitendo hicho kimeashiria Drake na Taylor kuwa na mahusiano huku kikiongezwa uzito na mwanadada Rihanna ambaye hakuhudhuria sherehe hizo.

Kwa mujibu wa chanzo kilichokaribu na Rihanna ambaye ndiye mpenzi wa Drake, ni kwamba alihuzunika baada ya Taylor kuonekana kuchukua nafasi yake kwa kuwa gumzo katika sherehe hiyo na kuwa staa huyo anajilaumu kwa nini hakuudhuria sherehe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *