Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana nchini Malta kujadili njia bora za kukabiliana na wimbi la uingiaji wa wahamiaji haramu kutoka Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

kikao hicho cha EU kinakuja kufuatia kauli ya waziri mkuu wa Italia, Paolo Gentiloni kuwa amefikia makubaliano na Libya ya namna ya kudhibiti wahamiaji wanavyotumia bahari kuingia Ulaya.

Waziri huyo mkuu ameahidi kutoa fedha zaidi na mafunzo kwa Libya kupambana na washabiashara haramu ya kuvusha watu.

Mamia ya maelfu ya wahamiaji huingia Ulaya kila mwaka ingawa wengi wao hufa kwa kuzama kwenye bahari ya Mediterranean.

Siku ya Alhamisi, walinzi wa pwani ya Italia walisema wamewaokoa zaidi ya wahamiaji 1,750 kutoka bahari ya Mediterranean ndani ya muda wa saa 24.

Libya imekosa uongozi imara na hali ya usalama na maisha imekuwa ngumu tangu nchi za Magharibi zilipouangusha kwa hila utawala wa hayati Muammar Gaddafi mwaka 2011.

‘Kama tunataka kuyapa nguvu na miguu ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji, inapaswa wanachama wote wa EU wakubali kutenga fedha,’ amesema Bw. Gentiloni.

Viongozi 28 wa mataifa washirika wa EU watajadili suala la mgogoro wa wahamiaji kwenye mji mkuu wa nchi ya Malta, Valletta baadae hii leo.

screen-shot-2017-02-03-at-09-07-21

Taarifa kwa hisani ya #bbc.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *