Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Halima Hassan amefariki dunia asubuhi hii baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo na figo.

Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamuziki Diamond Platinums, amethibitisha kifo cha mama yake kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Mama huyo alikuwa anapumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo.

Mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *