Aliyekuwa mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamuburo amefariki dunia leo ghafla katika hospitali ya KCMC mjini Moshi alipokuwa anapatiwa matibabu.

Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro, Bazil Lema amethibitisha kutokea kwa kifo hicho  cha mwanasiasa mkongwe nchini.

Lema amesema kuwa Ndesamburo alifika ofisini kwake kama kawaida leo lakini aliugua ghafla mida ya saa nne na nusu asubuhi na kukimbizwa hospitali ya KCMC ambapo alikutwa na umauti.

Katibu huyo wa Chadema wa Kilimanjaro amesema kuwa Ndesamburo alipoanza kujisikia vibaya alipelekwa katika hospitali ya KCMC na wakati madaktari wakiwa wanampatia matibabu ndipo alipofariki.

Lema amesema kuwa baada ya uchunguzi wa mwili wa marehemu ndiyo watajua ugonjwa uliosababisha kifo cha mwanasiasa huyo mkongwe nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *