Mwanamuziki mkongwe nchini Kenya, Achieng Abura amefariki dunia katika Hospitali taifa ya Kenyatta jijini Nairobi.

Achieng Abura pia aliwahi kuwa Principal kwenye mashindano ya Tusker Project Fame yanayofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Mwanamuziki huyo amefariki jana kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi mida ya saa 12 jioni.

Muimbaji huyo aliwahi kuandika kwenye mitandao ya kijamii kama afya yake si nzuri na madaktari walimshauri aongeze uzito kisha kuupunguza kupitia mazoezi.

Chanzo cha karibu na familia yake kilidai kuwa alihamishwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuwa mbaya.

Wasanii mbalimbali wa Kenya wametuma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *