Muigizaji wa Bongo movie, Kijakazi Pazi Shabani ‘Zamzam’ ambaye alipata umaarufu kupitia igizo la Kidedea amefariki dunia jana mkoani Kigoma.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo kutoka Kigoma kuelekea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi ambapo msiba huo utakuwa maeneo ya Sokota, Temeke karibu na sheli.

Kifo cha Zamzam kimekuja ikiwa ni siku chache baada ya mwigizaji Gift John ‘Hidaya’ kuaga dunia mnamo Desemba 29, 2016 katika Hospitali ya Sinza ‘Palestina’ na mwili wake kuagwa kwenye Kanisa la Anglikana lililopo Njiapanda ya Segerea, Dar juzi Jumamosi.

Zamzam alikuwa mwigizaji wa Kundi la Kidedea ambapo alijinyakulia umaarufu mkubwa baada ya kucheza tamthilia ya  Mchezo wa Kidedea, ambamo ndani yake aliigiza na marehemu Tabia huku baba yao alikiwa mzee Jengua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *