Muigizaji mkongwe wa Bollywood nchini India, Reema Lagoo amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na kifua.
Lagoo amefariki akiwa katika hospitali ya Dhirubhai Ambani baada ya kufikishwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Kabla ya umauti wake amekuwa akigiza mara nyingi kama mama kwenye filamu kama vile “Hum Aapke Hain Koun, “Kal Ho Na Ho pamoja na Kuch Kuch Hota Hai.
Lagoo mwenye miaka 59 kabla mauti kumfika, alifikishwa hospitalini hapo lakini alikuwa akilalamika juu ya maumivu makali ya kifua, Alisema msemaji wa Hospitali hiyo Bw. Ram Naraian.
Logoo amewahi kuigiza filamu kama vile “Maine Pyar Kiya”, “Saajan”, “Vaastav, na “Hum Saath-Saath Hain.