Aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ na klabu ya Yanga, Godfrey Bonny maarufu kama ‘Ndanje’ amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Godfrey Bonny amefariki dunia leo Jijini Mbeya alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu.

Taarifa za kuugua kwa kiungo huyo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu wakichangishana pesa kwa ajili ya kumsaidia mchezaji huyo kuendelea kupata matibabu katika hospitali hospitali ya Makandana iliyopo Tukuyu mkoani Mbeya.

Mchezaji huyo pia alicheza kwenye klabu ya Tanzanian Prisons ya mkoani Mbeya kabla ya kujiunga klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Tovuti hii itakuletea taarifa zaidi kuhusu shughuli za mazishi ya mchezaji huyo ambapo bado haijajulikana lini watampumzisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *