Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Mfaume amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo cha Dogo Mfaume aliyetamba na wimbo wake ‘Kazi ya Dukani’ zimetufikia hivi punde katika mtandao wetu.

Mwanamuziki huyo aliathirika na matumizi ya madawa ya kulevya mpaka kupelekea afya yake kudhoofika kutokana na madawa hayo.

Kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kukithiri kwa mwanamuziki huyo kumepelekea hadi kushuka kwa kipaji chake cha muziki kwa muda mrefu.

Mwanamuziki huyo pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards kutokana na wimbo wake wa ‘Kazi ya Dukani’.

Taarifa zaidi kuhusu kifo cha msanii huyo zitakujia endelea kusoma mtandao huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *